Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona ni mpana
2021-01-22 17:16:11| cri

Mshauri wa mambo ya uchumi wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni mshauri wa mambo ya uchumi wa kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa ECA Bw. Costantinos Bt. Costantinos, amesema ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye mapambano dhidi ya COVID-19 ni mpana.

Amesema vifaa vya matibabu vilivyotumwa na China kwenye nchi za Afrika vimekuwa msaada mkubwa kwenye nchi hizo, na karibu nchi zote zimepokea msaada wa vifaa vya kujikinga, na dawa za kutibu watu wenye dalili za COVID-19.

Bw. Costantinos ambaye pia ni profesa katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, amesisitiza kuwa uungaji mkono wa China katika kuziwezesha taasisi za afya barani Afrika ni muhimu kwa madaktari, manesi na wafanyakazi wa afya ili wawe na uwezo wa kudhibiti ugonjwa huo.