Kenya yasema uvamizi wa nzige wa jangwani sasa umedhibitiwa
2021-01-22 09:04:14| CRI

Wizara ya Kilimo ya Kenya imesema uvamizi wa wimbi la pili la nzige wa jangwani sasa umedhibitiwa kutokana na kuchukua hatua kwa wakati na madhubuti za kupambana nao.

Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika nchini Kenya Bw. Peter Munya amesema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwa sababu utayari wa serikali wa kukabiliana na janga la nzige umeimarishwa kwa kiasi kikubwa, na mpaka sasa hatua za kupambana nao zimeonesha ufanisi katika kaunti zote 15 walizovamia kutoka Ethiopia na Somalia tangu Novemba mwaka jana.