Kenya Aiways yaanza kutumia ndege za abiria kubeba mizigo
2021-01-22 18:29:08| cri

Shirika la ndege la Kenya Aiways imeendelea kutumia ndege zake za abiria kubeba mizigo kuziba pengo la uhaba wa abiria. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa shirika hilo, ndege kubwa za abiria Dreamliner zimegeuzwa kuwa za abiria.  Katibu mkuu mtendaji wa shirika hilo Allan Kilawuka amesema tayari wamesaini mapatano na wadau wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi.Ameongeza kuwa ndege hizo zina uwezo wa kufanya safari za mbali ikiwemo Marekani, Ulaya na Asia.Aidha Kilawuka ameongeza kuwa shirika hilo pia linalenga kununua ndege nyingine za mizigo ili kutosheleza ongezeko la mahitaji ya kusafirisha mizigo nje ya nchi.Shirika hilo limekuwa likilalamikia kudorora kwa soko katika Umoja wa ulaya na sehemu nyingine za dunia zinazochangiwa na masharti ya usafiri ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.