Mwanafunzi afukuzwa shule kutokana na kucheza simu ya mkononi darasani
2021-01-22 20:11:20| cri

Kadiri kiwango cha sayansi na teknolojia kinavyoinuka siku hadi siku, ndivyo wanafunzi wengi wana simu za mkononi, na ni hali ya kawaida kwa wanafunzi kuchezea darasani. Hivi karibuni mwanafunzi wa kidato cha pili kwenye sekondari ya juu mkoani Shanxi alifukuzwa shule kutokana na kuchezea simu ya mkononi darasani. Tukio hili limezusha mjadala mkubwa, na wanamtandao wengi wanaona adhabu hii ni kali kupita kiasi.

Baada ya tukio hilo kutokea Idara ya Elimu ya huko ilifanya uchunguzi kuhusu hali halisi na kufanya uratibu, na shule hiyo imeamua kufuta adhabu ya kumfukuza mwanafunzi huyo. Kiongozi wa shule hiyo ya sekondari ameeleza kuwa kanuni ya kupiga marufuku kuleta simu za mkononi darasani imewekwa miaka minne hadi mitano iliyopita, ambayo inalenga kuwadhibiti wanafunzi wasichezee simu za mkononi darasani, kanuni ambayo inakubaliwa na wazazi wengi.

Baadhi ya wanamtandao wanaona ni makosa kwa wanafunzi kucheza simu ya mkononi darasani, lakini kumfukuza shuleni ni adhabu kali kupita kiasi, kwani hili si kosa kubwa la wanafunzi, ni bora wawape fursa ili kukumbuka makosa yao.