Liverpool yafungwa nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne
2021-01-22 19:13:44| cri

Baada ya michezo 68, kushinda mara 55, na kutoka sare 13 kwa karibu miaka minne sasa, hatimaye Liverpool imefungwa kwa mara ya kwanza, na timu ambayo iko kwenye hatari ya kushuka daraja. Timu ya Burnley imeonekana kufanya maajabu yasiyotarajiwa na wengi, na ni mwezi uliopita tu waliicha Arsenal katika ushindi wa kwanza tangu mwaka 1974. Hii ni hali ya ajabu kwa Liverpool ambayo hakuna mtu anayejua sababu ya kukosa ushindi wakati iko katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi. Hadi sasa Liverpool haijafunga goli kwa jumla ya dakika 438 kwenye ligi, na imepata pointi tatu kati ya pointi 15 zilizowezekana, na sasa wanasubiri kwenda London kupambana na Tottenham, hali ambayo hakuna anayejua. Mara ya mwisho kwa Liverpool kuwa katika hali mbaya kama ya sasa ilikuwa ni mwaka 1999-2000 wakati wakiwa chini ya Gerald Houlier walicheza mechi nne bila ushindi.