Mashambulizi mawili ya mabomu mjini Baghdad yasababisha vifo vya watu 32 na wengine 110 kujeruhiwa
2021-01-22 08:55:10| CRI

Mashambulizi mawili ya mabomu mjini Baghdad yasababisha vifo vya watu 32 na wengine 110 kujeruhiwa_fororder_1127010702_16112442296541n

Mashambulizi mawili ya bomu yaliyotokea jana Alhamis katikati mwa Baghdad yamesababisha vifo vya watu 32 na wengine 110 kujeruhiwa na kuvunja utulivu wa miezi kadhaa katika mji mkuu huo wa Iraq.

Wizara ya mambo ya ndani kupitia msemaji wake Khalid al-Mahana ilitoa taarifa ikisema mlipuaji wa kwanza alililipua mkanda wa bomu kwenye soko la wazi la nguo za mitumba kwenye eneo la Bab al-sharji baada ya kudai anaumwa na watu kumzunguka ili kumsaidia. Mshambuliaji wa pili alijilipua dakika chache baadaye kwenye soko hilohilo wakati watu wamejikusanya ili kuwaondoa wahanga wa mlipuko wa mwanzo.