Karibu 90% ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaunga mkono vyuo vikuu kuanzisha somo la mapenzi
2021-01-22 20:44:05| cri

Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Lugha za kigeni cha Tianjin Lv Nannan ambaye amekuwa na mchumba akizungumzia somo la “saikolojia katika uhusiano wa mapenzi”, amesema alichagua somo hilo kutokana na mawazo ya “kutafuta upendo kwa kupitia kujifunza”, wakati ambapo bado hakujakuwa na uhusiano wa mapenzi. Amesema katika somo hili, ameelewa tofauti kati ya jinsia tofauti na jinsi wapenzi wanavyopaswa kuelewana, la muhimu zaidi ni kuwa baada ya kujifunza somo hilo, anaweza kuanzisha uhusiano wa mapenzi.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Madini, na mwalimu wa Somo la saikolojia ya mapenzi Duan Xinxing ameeleza kuwa, masomo kama hayo yameanzishwa kwenye vyuo vikuu vingi kote nchini.

Hivi karibuni, Shirikisho la vyombo vya habari vya vyuo vikuu likishirikiana na Gazeti la vijana wa China zimefanya utafiti kwa wanafunzi zaidi ya elfu moja, matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa, asilimia 88.23 ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaunga mkono somo la mapenzi kwenye vyuo vikuu. Miongoni mwa wanafunzi ambao walishiriki kwenye utafiti huo, asilimia 28.89 walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi, asilimia 37.55 wamekuwa na uzoefu wa kuwa na uhusiano wa mapenzi lakini sasa umevujika.

Bw. Duan Xinxin ameeleza kuwa aliandaa somo hili kwa wanafunzi kutokana na sababu mbili. Kwa upande mmoja ni kuwajulisha matukio mbalimbali mabaya yaliyosababishwa na matatizo yaliyoibuka kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kwa upande mwingine, kutokana na kuwa amegundua kuwa athari mkubwa zaidi kwa afya ya akili ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni uhusiano wa kihemko, ikiwa ni pamoja na uhusiano wa kifamilia, uhusiano kati ya watu, uhusiano wa mapenzi.

Katika uhusiano wa mapenzi, wanafunzi wa vyuo vikuu watakuwa na matatizo magumu au hali za kiakili ambazo ni vigumu kudhibiti. Utafiti umeonesha kuwa, namna ya kutatua migongano kwenye uhusiano wa mapenzi, na namna ya kukabiliana na kusimamishwa kwa uhusiano huo ni mambo ambayo wanafunzi wa vyuo vikuu wanayotarajia kujifunza kwenye somo la mapenzi.