Mwaka 2020 soko la fedha za kigeni la China ladumisha hali ya utulivu
2021-01-22 19:31:27| cri

Mwaka 2020 licha ya athari za janga la COVID-19 na hali yenye utatanishi mkubwa wa kimataifa, mzunguko wa fedha wa kuvuka mipaka ya nchi na soko la fedha za kigeni la China zimeshinda matatizo makubwa, na kupata ukuaji mzuri. Ofisa wa Idara ya Usimamizi wa fedha za kigeni ya China ameeleza kuwa, katika siku za baadaye, soko la fedha za kigeni litaimarisha hali ya uwiano kwa jumla na kubadilika katika kiwango mwafaka.

Mwishoni mwa mwaka 2020, kiwango cha ubadilishaji wa fedha za RMB dhidi ya Dola za kimarekani kiliongezeka kwa asilimia 6.9 kuliko mwaka 2019. Naibu mkurugenzi wa Idara ya usimamizi wa fedha za kigeni ya taifa Bibi Wang Chunying anasema:

 “Nchini China, hali ya kukinga na kudhibiti magonjwa inaendelea kuimarika, huku uchumi ukirejeshwa katika hali ya kawaida hatua kwa hatua. Vigezo vya biashara na nje, uwekezaji na matumizi pia vinadumisha hali ya utulivu na kupata mwelekeo mzuri. Wakati huo huo hali ya maambukizi ya virusi vya Corona katika nchi zilizoendelea duniani inazidi kuwa mbaya, uchumi unadorora, na vigezo vya dola za kimarekani vinashuka kwa haraka na kufikia kiwango cha chini zaidi katika miaka kadhaa iliyopita.”

Mwaka 2020, sarafu ya RMB ilidumisha hali ya utulivu ikilinganishwa na sarafu nyingine kubwa duniani. Bibi Wang Chunying ameeleza kuwa hivi sasa kiwango cha ubadilishaji wa RMB dhidi ya fedha nyingine za kigeni kinabadilika katika kiwango mwafaka, hakitaendelea kupanda bila ya kushuka au kudumisha kushuka bila kuongezeka. Anasema:

“Katika kipindi kijacho, Idara ya fedha za kigeni itashirikiana na Benki kuu ya China PBC, kudumisha kiwango cha ubadilishaji wa RMB dhidi ya fedha za kigeni katika kiwango mwafaka, kuendelea kuhimiza maendeleo ya soko la fedha za kigeni, na ufunguaji mlango na kuzisaidia kampuni kusimamia hatari kutokana na kiwango cha ubadilishaji wa fedha.”