Tedros aipongeza Marekani kwa kutoa ombi la kurejesha uanachama wake wa WHO
2021-01-22 09:03:37| CRI

Katibu mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus jana alhamisi alisema kuwa shirika lake linakaribisha ombi la Marekani la kujiunga tena na WHO.

Akiongea kwenye kikao cha 148 kinachoendelea cha Bodi ya Utendaji ya WHO, Bw. Tedros amesema WHO ni kama familia ya mataifa, hivyo wanafurahia kuona Marekani inabaki kwenye familia hiyo, na WHO inatarajia kuendeleza ushirikiano na Marekani kama nchi wanachama wengine.