Mji wa Changzhi wa mkoa wa Shanxi wahusisha matokeo ya upimaji wa maono na uzito katika matokeo ya jumla ya mtihani wa kuingia kwenye shule ya sekondari
2021-01-22 20:44:51| cri

Hivi karibuni, habari kuhusu mji wa Changzhi wa mkoa wa Shanxi kuhusisha matokeo ya upimaji maono na uzito katika matokeo ya jumla ya mtihani ya wanafunzi kuingia kwenye shule ya sekondari imezusha mjadala mkubwa.

Mwezi Juni mwaka 2019, mji huo ulitangaza kuwa kuanzia mwaka 2022, mtihani wa kuingia kwenye shule ya sekondari utaongeza alama 50 za tathmini za hali ya jumla za wanafunzi, zikiwa ni pamoja na alama 20 za sifa ya mwili.

Mkuu wa Idara ya elimu ya mji huo ameeleza kuwa, katika tathmini hizi mbili, hakuna tofauti kubwa katika alama za mwisho za wanafunzi. Lengo kuu la hatua hiyo ni kuwahamasisha wanafunzi kuimarisha mazoezi ya mwili na kulinda afya ya macho, ili kuongeza uwezo wa wa mwili.

Baadhi ya wanamtandao wanaona kuwa, kiwango cha maono kinategemea jeni za watu pamoja na tabia ya matumizi ya macho. Ingawa ni madhumuni mazuri kwa kuwahamasisha vijana kujenga tabia nzuri ya kutumia macho, lakini haifai kulinganisha kiwango cha maono na uzito na matokeo ya mtihani. Kwani mgawanyo wa maliasili ya elimu unatakiwa kuonesha utunzaji wa kibinadamu, ili kuwafanya watu wengi wapate usawa na haki.

Baadhi ya watu wanaona kuwa, kwa watu wenye uwezo mkubwa wa kiuchumi wanaweza kufanyiwa upasuaji wa macho ili kuboresha uwezo wa maono, lakini hii si haki kwa watu wenye matatizo kiuchumi. Wengine wanaona kuwa alama hata moja italeta matokeo makubwa ya mtihani wa wanafunzi, hivyo wana wasiwasi kuwa hatua hiyo italeta udanganyifu wakati wa utekelezaji.