FAO yazindua mradi wa kuimarisha usalama wa chakula nchini Somalia
2021-01-22 09:40:17| CRI

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limezindua mradi wa miaka mitatu nchini Somalia ili kuhimiza usalama wa chakula kwa kuongeza nafasi za kazi katika sekta ya uvuvi na mifugo.

Mwakilishi wa FAO nchini Somalia Bw. Etienne Peterschmitt jumatano jioni huko Mogadishu alisema kuwa mradi huo umepangwa kufanyika kote nchini Somalia hasa kwenye ushoroba wa Somaliland, Kaskazini ya Kati, Shabelle na Mto Juba.

Shirika la FAO linaona kuwa mradi huo utazingatia kuongeza kiwango, ubora na uthabiti wa uzalishaji, mauzo, kupanua upatikanaji wa masoko, na kuwajengea ujuzi na uwezo. Mradi huo unapanga kushirikiana na wafugaji, wavuvi, na wazalishaji wa asali kwa kutoa pembejeo za kilimo kama vile mbegu au zana pamoja na kusaidia katika mafunzo ya ufundi.