Afrika ya Kati yaingia kwenye hali ya dharura
2021-01-22 17:15:12| cri

Ikulu ya Afrika ya Kati imetangaza kuwa nchi hiyo imeingia kwenye hali ya dharura kwa siku 15 na kuruhusu idara husika kukamata watuhumiwa bila ya ruhusa kutoka mamlaka ya utekelezaji wa sheria ili kutuliza vurugu nchini humo.

Serikali ya nchi hiyo imelaani mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wanaojaribu kushambulia mji mkuu wa Bangui, kuwa ni jaribio la uasi la rais wa zamani wa nchi hiyo Bw. Francois Bozizé.

Habari zinasema balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia Afrika ya Kati kutuliza hali ya mvutano, kuongeza misaada na ushirikiano wa kimaendeleo.