China haikubali na haitasaini mkataba wa kupiga marufuku silaha za nyuklia
2021-01-22 19:53:41| CRI

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema, China haikubali na haitasaini au kuidhinisha mkataba wa kupiga marufuku silaha za nyuklia.

China imesisitiza kuwa mkataba huo hauonyeshi, pia hautakuwa sheria ya kimataifa, na hauna nguvu ya kisheria kwa nchi zisisosaini mkataba huo.

Bibi Hua Chunying amesema China inafahamu matumaini na matakwa ya nchi zisizo na silaha za nyuklia katika kuhimiza mchakato wa kupunguza silaha za nyuklia. Kuanzia siku ya kwanza ya kumiliki silaha za nyuklia, China inapendekeza kuzuia na kutokomeza kabisa silaha za nyuklia, na kushikilia msimamo wa kutotumia kwanza silaha za nyuklia wakati wowote na katika hali yoyote, imeahidi kutotumia silaha za nyuklia dhidi ya nchi zisizo na silaha za nyuklia na katika maeneo yasiyo na silaha hizo. China pia inadumisha nguvu yake ya nyuklia katika kiwango cha chini cha kulinda usalama wa taifa. Hizo zote ni sera za kimsingi ambazo serikali ya China inazishikilia.