Watu watano wafariki baada ya helikopta ya matibabu kuanguka Afrika Kusini
2021-01-22 09:04:42| CRI

Watu watano wafariki baada ya helikopta ya matibabu kuanguka Afrika Kusini_fororder_netcare-helicopter-crash-kzn-south-africa-696x464

Helikopta moja ya matibabu ya dharura ya Afrika Kusini ilianguka jana katika mkoa wa Kwazulu-Natal ulioko mashariki mwa nchi hiyo, na kusababisha vifo vya watu watano waliokuwa kwenye helikopita hiyo, wakiwemo rubani mmoja na wahudumu wanne wa afya.

Imeripotiwa kuwa helikopta hiyo ilianguka wakati ikiwa njiani kusafirisha mgonjwa mahututi kutoka mkoa wa Kwazulu-Natal kwenda Johannesburg. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.