Mwenyekiti wa Olimpiki asema michezo ya Olimpiki Japan itafanyika Julai kama ilivyopangwa
2021-01-22 19:14:10| cri

Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC, Bw. Thomas Bach, amesema Michezo ya Olimpiki itafanyika mwezi Julai licha ya hali ya hatari kutangazwa Tokyo kwa sababu ya kuongezeka kwa maambukizi ya Covid-19. Maoni ya umma nchini Japan kuhusu kupinga kufanyika kwa michezo ya Olimpiki yamekuwa yakiongezeka kutokana na hofu ya virusi lakini Bw. Bach amesema kwa sasa hakuna sababu yoyote ya kuamini kwamba Michezo ya Olimpiki huko Tokyo haitafunguliwa Julai 23 katika uwanja wa Olimpiki huko Tokyo. Amesisitiza kuwa hakuna mpango B ndio maana wamejiandaa kuhakikisha michezo inafanyika na kuhakikisha inakuwa salama. Hata hivyo alikumbusha kuwa kuna uwezekano wa kupunguza idadi ya watazamaji, na IOC inapaswa kubadilika na inaweza kuhitaji kujitolea ili kulinda maisha ya watu watakaoshiriki.