Maonyesho ya nne ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa ya China yafanya shughuli ya matangazo kwenye mtandao wa Internet
2021-01-22 19:57:47| cri

Maonyesho ya nne ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa ya China CIIE yamefanya shughuli ya kwanza ya matangazo kwenye mtandao wa internet kwa ajili ya makampuni ya nje, na kuvutia makampuni ya Ujerumani zaidi ya 100.

Mkurugenzi wa idara ya maonyesho hayo Bw. Liu Fuxue amesema waandaaji wanafanya juhudi ya kuyaalika makampuni ya nje kupitia shughuli za matangazo kwenye mtandao wa Internet, ili kuepusha madhara ya COVID-19 kwa maonesho hayo.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya AHK China Bw Jan Jovy amesema maonyesho ya CIIE yameonekana kuwa jukwaa muhimu kwa makampuni mbalimbali duniani kuonyesha ujuzi wao kwenye soko la China.

Kwenye maonyesho ya mwaka jana makampuni zaidi ya 170 ya Ujerumani yalishiriki kwenye maonyesho, yakiwa na eneo lenye ukubwa wa mita za mraba elfu 18, idadi zote mbili zikiwa kubwa kuliko nchi zile za Ulaya.