Je ni hatua mwafaka kwa kuwazuia wagonjwa wa sonona kupanda ndege
2021-01-25 20:57:17| cri

Hivi karibuni, msichana mmoja mwanafunzi wa Chuo Kikuu akifuatana na mchumba wake Bw. Yu, walijiandaa kupanda ndege kutoka mji wa Weihai kwenda mji wa Nanjing kwa ajili ya matibabu. Lakini msichana huyo alikataliwa kupanda ndege kwa sababu mikono yake ilikuwa inatetemeka kutokana na kutumia dawa za sonona. Iliwabidi watu hao wawili waende Nanjing kwa treni ya mwendo kasi usiku kucha.

Hivi sasa wamewasilisha malalamiko kwa mamlaka ya usafiri wa ndege wa umma, ili kutaka waombwe msamaha na kulipwa fidia. Wafanyakazi wa huduma za wateja wa Shirika la ndege wameeleza kuwa sonona ni aina moja ya ugonjwa wa kiakili, na wagonjwa wakihitaji kupande ndege, wanapaswa kuonesha kitambulisho kutoka hospitali, na shirika la ndege litaamua kama wataweza kupanda ndege au la.

Hali kama hayo si chache. Kadiri jamii inavyozidi kupata maendeleo, ingawa kiwango cha maisha ya watu kimekuwa kikiinuka, lakini uwezo wa watu wa kukabiliana na shinikizo unazidi kupungua, hali ambayo imesababisha watu wengi zaidi kukumbwa na matatizo ya kiakili.