Chuo Kikuu cha Hehai chafukuza wanafunzi 125 washahada ya udaktari
2021-01-28 19:55:27| cri

Hivi karibuni, Chuo Kikuu cha Hehai kilitangazakuwafukuza wanafunzi 125 wanaosomea shahada ya udaktari ambao hawajapata shahada na kuhitimu ndani ya muda uliowekwa, na kusema kuwa wanafunzi hao wanaweza kukata rufaa ndani ya siku 10 kama wanaona wameonewa.

Katika miaka ya hivi karibuni, vyuo vikuu mbalimbali vya China kikiwemo Chuo Kikuu cha Wanaanga cha Beijing , Chuo Kikuu cha Zhongshan, na Chuo Kikuu cha Kaskazini Mashariki, vyote vimetangazakuwafukuza wanafunzi wanaosomea shahada ya juu.

Wasomi wanaona kuwa kuanzishwa kwa utaratibu wa kuweka mipaka mikali juu ya wahitimu itaweza kuzuia matumizi mabaya ya rasilimali za elimu na kuimarisha ubora wa elimu ya wahitimu.