Mfanyakazi afukuzwa kazi kwa kuomba likizo ya siku nane baada ya baba yake kufariki
2021-01-28 19:54:17| cri

Bw. Lu Yunsheng ni mfanyakazi wa kampuni ya mali mjini Shanghai. Januari 6 mwaka jana, alirudi nyumbani kwao baada ya kuwasilisha fomu ya ombi la likizo kwa msimamizi wake kwa sababu alikuwa akiuguliwa na baba yake. Siku iliyofuata, Bw. Lu alirudi kazini kwa kuwa kampuni yake haikumruhusu aende likizo. Lakini alipokuwa njiani akirudi kazini kwake alipata taarifa kuwa baba yake amefariki dunia hivyo aligeuza safari na kurudi tena nyumbani kwao kushughulikia mambo ya mazishi. Januari 14 mwaka 2020, Bw. Lu alirudi Shanghai na kuanza kazi siku iliyofuata.

Tarehe 31 Januari, kampuni hiyo ilitoa taarifa ya kusitisha Mkataba wake wa kazi.