Wizara ya Elimu yatoa waraka wa kukagua kwa pande zote hali ya udhalilishaji na uonevu shuleni
2021-02-02 20:46:12| cri

Katika muda mrefu uliopita, vitendo vya uonevu vimekuwa vikitokea mara kwa mara, na wahanga wengi walivumilia bila ya kuwaambia wazazi na walimu wao, lakini hali kama hii imewasumbua vibaya.

Katika miaka ya hivi karibuni, kuna matukio mengi ya uonevu yanayoripotiwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari: Msichana mwenye umri wa miaka 15 wa shule ya sekondari alimshambulia msichana mdogo; na mwanafunzi wa miaka 15 katika shule ya ufundi alishambuliwa kwa kuvuliwa nguo mbele ya wanafunzi wenzake… Matukio kama hayo yanafuatiliwa sana na watu.

Hivi karibuni Wizara ya Elimu imezindua operesheni ya usimamizi ya miezi sita juu ya hali ya udhalilishaji katika shule za msingi na sekondari, kuchunguza kwa kina vitendo vya udhalilishaji, kuanzisha na kuboresha mfumo wa kuripoti vitendo vya udhalilishaji wa wanafunzi, kuhusisha kazi ya kuzuia vitendo vya udhalilishaji katika mfumo wa tathmini ya kazi ya walimu, na kuwapeleka wanyanyasaji sugu ambao hawajirekebishi kwenye shule maalumu.