Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC Bw. Thomas Bach hivi karibuni ameeleza kuwa, maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing inaendelea kwa utaratibu, na ana imani kubwa na mafanikio ya michezo hiyo.
Bw. Bach amesema hayo alipofanyiwa mahojiano na mwandishi wa habari wa Shirika la Kuu la Utangazaji la China CMG.
Katika mahojiano hayo Bw. Bach ameisifu China kwa kuitoa michezo na Michezo ya Olimpiki kwenye janga la virusi vya Corona, pia amemshukuru rais Xi kwa kuiunga mkono michezo hiyo.