Wawaume wanne wamaliza kula kilo 30 za machungwa ndani ya nusu saa ili kuepuka kulipa gharama ya uchukuzi
2021-02-03 15:45:27| cri

Hivi karibuni, Bw. Wang na wenzake watatu kutoka mji wa Kunming mkoani Yunan walipokuwa kwenye safari ya kikazi kwenye mji mwingine, walitumia yuan 50 kununua boksi moja la machungwa kabla ya kurudi, lakini walipokuwa uwanja wa ndege waliambiwa kuwa wanatakiwa kulipa yuan 300 kama gharama ya kusafirisha machungwa hayo, kwa hivyo waliamua kuyala yote papo hapo.

Bw. Wang alisema kuwa wao wanne walitumia nusa saa tu kumaliza machungwa hayo ya kilo 30, na kwamba hataki kula matunda hayo tena katika maisha yake yote.

Video yao imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii na wanamtandao wakatoa mapendekezo yao ili kuepuka gharama hiyo ya usafirishaji.

Mwanamtandao mmoja alisema wanaweza kugawa machungwa hayo kwa wapita njia, na hakuna haja kabisa ya kujitesa namna hii.

Mwingine alisema wanaweza kununua mifuko kadhaa ya plastiki, na kila mmoja abebe machungwa kadhaa, kwa kuwa kila abiria anaruhusiwa kubeba mzigo kiasi bila malipo.