Mkutano wa waziri wa fedha wa UNECA kujadili COVID-19 na eneo la biashara huria la Afrika
2021-02-04 09:14:52| CRI

Mkutano wa mawaziri wa fedha, mipango na maendeleo ya uchumi wa nchi za Afrika utakaofanyika chini ya kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA, unalenga kujadili Eneo la Biashara huria la Afrika (AfCFTA) na mapambano dhidi ya COVID-19.

Mkutano huo utafanyika mjini Addis Ababa kati ya Machi 17-23 kwa kauli mbiu ya “maendeleo endelevu ya viwanda barani Afrika na kuwa na vyanzo mbalimbali katika zama ya COVID-19.

Ofisa mwandamizi wa UNECA Bw. Stephen Karingi amesema kauli mbiu hiyo imekuja kwa wakati, hasa ikizingatiwa kuwa inatoa jukwaa kwa mawaziri na watalaam kujadili mahitaji ya kuhakikisha mikakati ya kidigitali inakuwa na sera za pamoja na kupanga mipango ya utekelezaji wa maendeleo ya viwanda.

Taarifa iliyotolewa na UNIECA pia imesema kuanza kutekelezwa kwa eneo la biashara huria barani Afrika ni ishara ya hatua muhimu kwa bara la Afrika kuhimiza maendeleo ya viwanda, biashara kwa njia ya mtandao wa internet, nyenzo muhimu ya uchumi wa kidigitali, na pia ni hatua muhimu kwa maendeleo ya miundo mbinu.