Serikali ya China yapunguza muda wa kusambaza vifurushi wakati wa baridi kali ili kuhakikisha usalama wa wasambazaji vifurushi
2021-02-05 15:45:55| cri

Hivi karibuni Wizara ya Rasilimali Watu na Usalama wa Jamii na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi la China wametangaza kwa pamoja waraka unaozielekeza kampuni kurekebisha muda wa kazi, kuongeza nguvu katika kubadilisha zamu ya wafanyakazi, na kupunguza kiwango cha kazi, ili kuwapunguzia muda wafanyakazi wanaofanya kazi nje ya nyumba wakati wa baridi kali.

Waraka huo pia unaziagiza kampuni kutowapunguzia mishahara wafanyakazi wakati muda wao unapopunguzwa kutokana na baridi kali, na kutoa posho kwa wale wanaofanya kazi wakati kama huo. Vilevile unazihimiza kampuni kuwapa mshahara mkubwa zaidi watu wanaofanya kazi katika mstari wa mbele, na kazi ngumu, kuzidi kuboresha mazingira yao ya kazi, na kuwaongezea mishahara.