Huduma za kuwatunza wazee katika nyumbani zaanzishwa kwa majaribio mjini Hangzhou
2021-02-08 18:25:29| cri

Hivi karibuni mitaa minane mjini Hangzhou ilianza huduma za kuwatunza wazee nyumbani kwa majaribio, hatua ambayo itawafanya wazee wengi zaidi kupata huduma bora za mashirika ya matunzo ya wazee katika nyumba zao.

Huduma hizo ni pamoja na huduma za maisha, usimamizi wa afya, matibabu na matunzo, msaada wa kisaikolojia, burudani pamoja na huduma nyingine.

Majaribio hayo yataendelea kwa miaka miwili, na wazee ambao wana umri wa miaka zaidi ya 60 ambao upimaji wa uwezo wao umefikia kiwango cha katikati na cha juu cha ulemavu, au umri wao umezidi miaka 80, wanaweza kuomba huduma hizo. Wenye matatizo ya kiuchumi wanaweza kutangulia kupewa huduma kama hizo kutegemea maombi yao au ya jamaa zao. Na serikali itatoa ruzuku isiyozidi dola za kimarekani mia moja kwa mtu mmoja kila mwezi.