Wanakijiji wasiotaka kwenda sehemu nyingine kufanya kazi wawekwa katika “orodha nyeusi”
2021-02-08 18:20:51| cri

Hivi karibuni taarifa ya kijiji kimoja mkoani Yunnan imetangaza “orodha nyeusi” yenye majina ya wanakijiji wasiotaka kwenda sehemu nyingine kutafuta ajira, hali ambayo imefuatiliwa na watu. Bw. Zhou na baba yake wamewekwa kwenye orodha hiyo kutokana na “kutotaka kwenda nje kutafuta ajira na kufanya uvivu kwa kisingizio cha janga la Corona”.

Bw. Zhou amesema kutokana na kuwa baba yake alikuwa mgonjwa, mwaka jana alitoka nje mara tatu kufanya kazi. Pia amesema tangu alipojua kuwa ameorodheshwa kuwa mvivu, alikwenda kuwasiliana na maofisa wa kijiji, lakini hakupata ufafanuzi mzuri. Mwezi Februari mwaka huu, Kamati ya Kijiji ilimwomba msamaha mwanakijiji huyo, ikisema hatua hii haikufanyika kwa kufuata vigezo mwafaka.

Tukio kama hilo kweli limeonesha matatizo mengi yakiwemo matumizi mabaya ya nguvu yaliyooneshwa kwenye “orodha nyeusi’. Ingawa orodha kama hii si adhabu kali, lakini ni matusi makubwa kwa watu. Hamna mtu anayependa kutajwa kuwa mvivu, sembuse Bw. Zhou ambaye kweli si mvivu. Kwa upande wa kamati ya kijiji, ilisema ilifanya uhamasishaji mara nyingi wakati wa kuweka orodha hiyo, lakini wakati Bw. Zhou alipowasiliana na kamati ya kijiji, kamati hiyo haikutoa majibu hadi tukio hili liliposambaa kwenye mtandao wa Internet.