Gym ndogo zinazohamishika zafunguliwa rasmi Shanghai
2021-02-08 15:45:10| cri

Kutokana na umma kuwa na mwamko zaidi wa kushiriki kwenye mazoezi ya viungo, imekuwa tabia ya kiafya na kisasa ya kufanya mazoezi kwenye gym. Lakini wakati huohuo, watu wengi wanaenda gym mara chache tu kila mwaka baada ya kulipa ada kubwa ya uanachama.

Hivi karibuni, gym ndogo zinazohamishika zinazoitwa “Shared Gym” zimefunguliwa rasmi mjini Shanghai. Gym hizo hazihitaji malipo ya uanachama, mtu yeyote anaweza kuingia na kufanya mazoezi kwa kuscan kwa simu barcode iliyobandikwa mlangoni, na gharama zinahesabiwa kutokana na muda wa matumizi.

Imefahamika kuwa bei ya kutumia Gym hizo ni yuan mbili kwa saa kuanzia saa moja hadi saa nne asubuhi, yuan tano kwa saa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 12 jioni, na yuan 8 kwa saa kuanzia saa 12 jioni hadi saa 4 usiku.

Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa biashara ya kielektroniki ya mji wa Ningbo Bw. Lin Chengliang anaona ni jambo zuri kuingiza mifumo ya kidijitali kwenye gym, na pia ni jaribio jipya la dhana ya “Sharing Economy” kwenye sekta ya mazoezi ya mwili.