Tukio la nyota kuwaajiri wengine kubeba ujauzito lafuatiliwa na jamii
2021-02-09 15:45:32| cri

Hivi karibuni, mwigizaji nyota wa kike wa China Zheng Shuang na mpenzi wake wa zamani Zhang Heng wameshukiwa kuwaajiri watu wengine kuwazalia watoto wawili, na “kutaka kuwaacha”, tukio ambalo limezusha mjadala mkali. Baada ya hapo Zheng Shuang alijibu kuwa, jambo hilo “lilifichuliwa hatua kwa hatua kwa nia mbaya”, na kwamba “hakwenda kinyume na sheria, na pia aliheshimu sheria na kanuni zote nje ya nchi”. Tukio hilo bado limepata maendeleo mapya, na hali ya “kuwaajiri wengine kubeba ujauzito na kuzaa watoto” imekuwa inafuatiliwa sana na watu .

Kuna uvumi mwingi wa waigizaji kuwajiri wengine kuwazalia watoto, hata baadhi wanajitangaza hadharani kuwa wanahifadhi mayai yao ili kujiandaa kuwaajiri wengine kuwazalia watoto katika siku za baadaye. Kuna misimamo tofauti kwa nchi mbalimbali juu ya hali ya kuwaajiri wengine kubeba ujauzito, yaani kupiga marufuku, uhalali na kuruhusu hali ya kuwasaidia wengine kubeba ujauzito kwa kujitolea.

China inapiga marufuku aina zote za kuwaajiri wengine kubeba ujauzito. “Kanuni za usimamizi wa teknolojia ya usaidizi wa uzazi wa Binadamu” zinasema wazi kuwa, ni marufuku kununua au kuuza uja uzito katika hatua yoyote na kwa njia yoyote. Mashirika ya matibabu na wafanyakazi wao hawapaswi kutekeleza aina yoyote ya teknolojia ya aina hii.