Mawaziri wa fedha wa Afrika wakutana na wakuu wa UNECA na IMF kujadili mwitikio wa COVID-19 kiuchumi
2021-02-10 09:35:14| CRI

Mawaziri wa fedha wa Afrika wamekutana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Kiuchumi ya Umoja wa Mataifa katika Afrika UNECA Vera Songwe pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani IMF Kristalina Georgieva na kujadili mwitikio wa haraka wa kiuchumi katika janga la COVID-19.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNECA, mawaziri hao walitoa wito wa pamoja juu ya kuongeza upatikanaji wa fedha dola za kimarekani bilioni 500 katika Hifadhi ya Mali ya Kimataifa (SDR), upatikanaji mzuri wa soko, kuongeza rasilimali zenye masharti nafuu na kuongeza muda katika Mpango wa Huduma ya Kusitisha Madeni DSSI, kutokana na janga kuendelea kwa muda mrefu.

Kwenye mkutano huo uliofanyika Februari 5 Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Ghana Ofori-Atta alisema athari za janga la COVID-19 ni jambo la kutisha kwa waziri yeyote wa fedha akishuhudia huku akiwa hana njia ya kusaidia.