Taakwimu za benki kuu ya kenya zinaonesha kuwa matumizi ya kadi kama vile ATM na nyinginezo kufanya malipo au biashara yamepungua mwaka 2020 kutokana na hatua za kukabili kuenea kwa virusi vya corona.
Taakwimu hizo zinaonesha kuwa pesa zilizotumika kwa njia ya kadi kama hizo mwaka 2020 ni dola bilioni 1.43 ikilinganishwa na dola bilioni 1.49 za awali.
Hiyo ilikuwa upunguaji wa karibu dola milioni 54 ikiwa pia ni wa kwanza kushuhudiwa ndani ya miaka 5.
Hatua za kukabili COVID-19 ambazo Kenya ilianzisha Machi 2020 zilijumuisha ufungaji na kuzuia kuingia ndani na nje ya mji mkuu Nairobi na miji mingine mikubwa, kufungwa kwa hoteli na baa na kuwekwa kwa amri ya kutotoka nje.
Wakati matumizi ya kadi yakipungua, hata hivyo, utumaji na ulipaji wa pesa kwa njia ya simu uliongezeka na kufikia dola bilioni 47.3.