Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa China laonesha uzuri wa zama mpya na kuongeza imani na shauku ya watu kwa mwaka ujao
2021-02-12 17:19:16| CRI

Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa China laonesha uzuri wa zama mpya na kuongeza imani na shauku ya watu kwa mwaka ujao_fororder_003PjSf0ly1gnk2ty6sv7j61ej0u0b2c02

Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa China lililoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG lilifanyika jana usiku, likifanikiwa kujumuisha mambo ya kifikra, kisanaa na kiuvumbuzi, na kupongezwa na watazamaji na vyombo vya habari kuwa ni tafrija kubwa ya kiutamaduni kwa wachina kote duniani. 

Takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia jana saa sita usiku, idadi ya watazamaji wa Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa China ilifikia bilioni 1.14, kati ya watamazaji hao, milioni 569 walitazama kwa njia ya mtandao, huku wengine milioni 571 wakitazama kupitia televisheni.

Ngonjera fupi ya kuchekesha (short sketch) inayoitwa “Roshani” ambayo ilionesha wachina walivyojaliana na kusaidiana kwenye mapambano ya taifa dhidi ya janga la virusi vya Corona, yamewagusa sana wahudumu wa afya waliokuwa kmstari wa mbele kwenye mapambano hayo, mmojawao ni Bibi Shao, aliyekuwa na haya ya kusema,

“Nikiwa ni mhudumu wa afya, nimewahi kushiriki kwenye kampeni ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, maigizo haya yamenikumbusha tulivyoshikamana na kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya janga hili. Najivunia kuweza kuwa mhudumu wa afya.”

Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa China laonesha uzuri wa zama mpya na kuongeza imani na shauku ya watu kwa mwaka ujao_fororder_003PjSf0ly1gnk2p0em5xj61ej0u04qp02

Tamasha la mwaka huu pia ni tafrija inayojumuisha teknolojia nyingi za hali ya juu, ikiwemo video ya 8K, Studio ya kisasa inayotumia Akili Bandia (AI) na VR 3D (Autostereoscopy), na teknolojia ya Cloud Video. Maonesho ya mitindo ya mavazi yanayoitwa “Shan Shui Ni Chang” yalitumia teknolojia za kisasa za kamera na picha na kuonesha urembo wa mavazi wa kichina. Mtazamaji Bibi Shi anasema:

“Maonesho haya yameunganisha teknolojia za kisasa, historia, utamaduni na urembo wa mavazi, kweli yamenipendekeza sana.”

Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa China laonesha uzuri wa zama mpya na kuongeza imani na shauku ya watu kwa mwaka ujao_fororder_003PjSf0ly1gnk1lda9c6j61ej0u0e8302

Tamasha la Mwaka Mpya wa Jadi wa China ni tafrija ya kiutamaduni isiyokosekana kwenye sikukuu hii kubwa ya kujumuika kwa familia za wachina. Tamasha hilo limefanyika kwa miaka zaidi ya 30 mfululizo tangu mwaka 1983, na limethibitishwa kuwa ni kipindi cha televisheni chenye watamazaji wengi zaidi duniani katika rekodi za dunia za Guinness.

Tamasha hilo la mwaka huu pia limewavutia wageni wengi walioko China. Mwanafunzi kutoka Tajikistan Kamolov Mahmadovich, amesema anapenda zaidi maonesho yanayoonesha utamaduni wa kichina.

“Ninayopenda zaidi ni maonesho ya mitindo ya mavazi ya kichina ‘Shan Shui Ni Hong’, nimeona mavazi mengi yenye utamaduni wa kichina, napenda sana mavazi yenye rangi ya nyekundu ya kichina, kwa kuwa yanaongeza shamrashamra za sikukuu ya mwaka mpya.”Bibi Pronkina Olga ni mwalimu kutoka Russia anayefundisha mkoani Gansu. Amesema amefurahi kuona ngoma za kirussia kwenye tamasha la mwaka mpya wa kichina. Anasema,

“Wakati nilipoona ngoma za kirussia nilikuwa nakumbuka sana maskani yangu. Nawapongeza wachezaji wa China kwa kuwa walicheza vizuri ngoma ya Gopak ambayo ni ngumu sana. Natumai kuwa katika matamasha yajayo nitaweza kuona wachezaji wa China na Russia wakicheza ngoma kwa pamoja.”Vyombo vya habari zaidi ya 600 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 170 zikiwemo Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Russia, Japan, Brazil, Australia, India, UAE, Malaysia na Afrika Kusini, vilitangaza moja kwa moja tamasha hilo.