Chombo cha China cha utafiti wa sayari ya Mars Tianwen-1 chafanya marekebisho kwenye njia yake ya obit
2021-02-15 19:09:29| CRI

Chombo cha China cha utafiti wa sayari ya Mars Tianwen-1 chafanya marekebisho kwenye njia yake ya obit_fororder_9345d688d43f8794f658efae0db003fc1ad53a3a

Chombo cha China cha utafiti wa sayari ya Mars Tianwen-1 kimefanya marekebisho ya njia yake ya obit, kikiwa ni chombo cha kwanza cha China kufanya uchunguzi kwenye sayari ya Mars.

Idara ya safari za anga ya juu ya China imesema moja ya injini zake ziliwashwa kuhakikisha njia yake inapita kwenye ncha ya sayari ya Mars. Sehemu ya obit ambayo iko karibu zaidi na sayari ya Mars ilirekebishwa kuwa kilometa 265, na kutakuwa na marekebisho zaidi ili kiende kwenye obiti nyingine. Chombo hicho kinatarajiwa kutua kwenye sayari ya Mars  kati ya mwezi Mei na Juni.