Chanjo ya COVID-19 iliyotolewa na China yafika Zimbabwe
2021-02-15 18:32:38| CRI

Chanjo ya COVID-19 iliyotolewa na China yafika Zimbabwe_fororder_微信图片_20210215160840

Leo Saa 11 na dakika 40 alfajiri kwa saa za Zimbabwe, ndege maalumu ya kusafirisha chanjo ya COVID-19 iliyotolewa na China kwa Zimbabwe imefika uwanja wa ndege ya kimataifa ya Harare.

Makamu rais wa Zimbabwe Bw. Constantino Chiwenga, na maofisa wengine wa nchi hiyo wamekwenda Uwanja wa ndege kupokea chanjo hiyo.

Bw. Chiwenga amesema kwa muda mrefu uliopita, China inaendelea kutoa msaada kwa Zimbabwe kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, chanjo hizo iliyotolewa na China itatoa mchango kwa Zimbabwe kukabiliana na janga hilo na kurejesha uzalishaji na maisha ya kawaida.