Zimbabwe : Zimbabwe kusaini mkataba wa kuuza matunda kwenye soko la China
2021-02-17 17:31:30| CRI

Zimbabwe inatarajiwa kusaini mkataba wa kuanza kuuza matunda kwenye soko la China ambao utawapa wakulima wa ndani ufikiaji wa moja kwa moja kwa soko lenye thamani ya dola milioni 500 za kila mwaka.

Kulingana na wakala wa nchi hiyo wa maendeleo na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, ZimTrade, sasa serikali inafanya mazungumzo na mamlaka husika ya China na kuutaja mpango huo  kama utakaobadilisha sekta ya kilimo.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZimTrade Allan Majuru alisema mpango huo mpya unatarajiwa kufungua ufikiaji wa moja kwa moja kwa soko kubwa kwa wakulima ambao hapo awali walitegemea soko la tu soko la Ulaya.

Matunda yatakayouzwa kwenye soko hilo la China ni  pamoja na machungwa, mandarin, ndimu, limau, na zabibu.