SOKA: Biashara United Mara kulipa kisasi?
2021-02-17 16:11:53| CRI

Biashara United Mara imejizatiti kuwakabili vilivyo Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, katika mchezo wa mzunguuko wa 20 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho. Simba SC Jumatatu ilianza mandalizi jijini Dar es salaam, baada ya mapumziko ya siku moja, na jana imeondoka jijini humo kueleka Musoma, Mara kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa. Simba SC inakwenda kwenye mchezo huo huku ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuanza vyema michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuifunga AS Vita Club ya DR Congo, bao 1-0 mwishoni mwa juma lililopita.