SOKA: Pogba kuwa nje kwa wiki mbili zaidi
2021-02-17 16:12:48| CRI

Klabu ya Manchester United ina wasiwasi kuwa nyota wake Paul Pogba huenda akawa nje ya uwanja kwa wiki mbili zaidi kutokana na jeraha la paja alillolipata hivi karibuni. Tayari mchezaji huyo amekosa mechi mbili zilizopita kutokana na tatizo hilo, na anaweza kukosa mechi nyingine tatu zijazo. Klabu ya Man United imesema inatumai kuwa huena Pogba akacheza kidogo kwenye mechi ijayo katika uwanja wa Stamford Bridge.