Tanzania: Coca-Cola yazindua kampeni ya kutambua wanawake
2021-02-17 17:30:22| CRI

   Kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola nchini Tanzania imezindua kampeni ya kumtambua mwanamke shujaa kwa lengo la kutambua mchango mkubwa unaofanywa na wanawake hao katika kuliletea taifa maendeleo.

Imezindua kampeni hiyo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 3, kila mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Mauzo Coca-Cola Kwanza, Josephine Msalilwa, alisema lengo la kampeni hiyo ni kusherehekea, kutambua na kuhamasisha wanawake kutoka katika sekta mbalimbali kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Pia, alisema katika kutambua mchango kwa wanawake hao, watatoa tuzo kwa wanawake wanaofanya vizuri katika sekta mbalimbali hususani katika nafasi za uongozi.