Ethiopia : Kampuni za China na Korea Kusini zasaini mkataba wa umeme na Ethiopia
2021-02-17 17:32:36| CRI

Serikali ya Ethiopia imetia saini kandarasi ya mradi wa umeme wa dola milioni 24 na kampuni tatu za China na kampuni moja ya Korea Kusini.

Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Shirika la Umeme la Ethiopia (EEU), Melaku Taye, amesema mradi huo unakusudia kufikisha umeme katika miji 25 kote nchini, ambayo inatarajiwa kufaidi watu wapatao 145,000.   

Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali ya Ethiopia zinatarajiwa kugharamia kwa pamoja gharama ya jumla ya mradi huo.

Serikali inapanga kuongezea upatikanaji wa huduma za umeme kote nchini humo kutoka karibu asilimia 60 kwa sasa hadi asilimia 100 ifikapo 2025.