Namba za Ushiriki Kili Marathon Kutolewa Mlimani City
2021-02-18 15:28:47| cri

Waandaaji wa mbio maarufu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2021 zitakazofanyika wiki ijayo mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro wametangaza kituo kitakachotumika kuchukua  namba za ushiriki kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyotoelwa na kamati ya maandalizi ya mbio hizo za kimataifa, zoezi hilo litafanyika katika sehemu ya kupaki magari katika viwanja vya Mlimani City, karibu na mgahawa wa Pizza Hut siku ya Jumamosi na Jumapili wikiendi hii kuanzia saa sita mchana mpaka saa kumi na mbili jioni.

Walisema kuwa zoezi la kujiandikisha kwa mbio za kilomita 42 na zile za kilomita 5 kwa ajili ya kujifurahisha linaendelea katika vituo vya kuchukulia namba lakini litafanyika kwa malipo ya papo kwa papo ila zoezi hilo limefungwa kwa wale wanaotaka kukimbia mbio za kilomita 21.