Ngorongoro Heroes yaanza vibaya michuano ya Afcon u20 Mauritania, yacharazwa 4-0 na Ghana
2021-02-18 15:28:25| cri

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imeanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa kwa Vijana chini ya umri wa miaka 20, (AFCON U20) baada ya kuchapwa 4-0 na Ghana usiku wa juzi Uwanja wa Manispaa ya Nouadhibou Jijini Nouadhibou nchini Mauritania.

Katika mchezo huo wa Kundi C, mabao ya Ghana yalifungwa na Percious Boah dakika ya tatu na 71, Abdul Fatawu Issahaku dakika ya 30 na Joselpho Barnes dakika ya 89 – wakati mechi nyingine ya kundi hilo a, Morocco iliichapa Gambia 1-0, bao pekee la El Mehdi Moubarik dakika ya 26.  Baada ya mchezo huo, kocha wa Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema ugeni wa mashindano ndiyo ulisababisha wafungwe 4-0 na Ghana.