NCBA yakadiria uchumi wa Kenya kukua kwa 4.9%
2021-02-18 19:56:49| cri

Benki ya NCBA inakadiria kuwa uchumi wa Kenya utakua kwa asilimia 4.9 huu mwkaa kufuatia kupunguzwa kwa vikwazo vya mlipuko wa korona .

Utabiri wa benki hiyo hata hivyo uko chini ya ule uliotolewa na Wizara ya Fedha na Benki ya Dunia.

Wizara ya Fedha na Benki ya Duynia zilitabiri kuwa ukuaji wa uchumi utafufuta kutoka asilimia 0.6 mwaka jana hadi aslimia 6.4 na asilimia 6.9.

Kulingana na Benki ya Dunia,pato la Taifa a Kenya litakuwa juu ukilinganisha na mataifa mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,huku uchumi wa Rwanda ukitarajiwa kukua kwa asilimia 5.7,Tanzania kwa asilimia 5.5,Uganda asilimia 2.8 ,Burundi asilimia 2 na Sudan Kusini asilimia 3.

Katika mtazamo wake mpya wa kiuchumi ,NCBA inaonya kuwa ufufukaji wa uchumi utahitaji hatua bora zitakazochukuliwa na serikali.