Uganda-UNBS yatoa onyo kwa watengezaji maski zisizokidhi viwango
2021-02-18 19:57:47| cri

Wakati makampuni mengi yakijiingiza katika utengenezaji wa maski,Shirika la kukagua Ubora wa Bidhaa la Uganda (UNBS) limetoa onyo dhidi ya usambazaji maski zisizokidhi viwango.

Kulingana na UNBS ,baadhi ya watengenezaji bidhaa hiyo wameharakisha mchakato huo kutokana na hitaji la bidhaa hiyo hasa wakati huu ambpao baadhi ya wanafunzi wanatarajiwa kurudi shuleni.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau uliojumuisha watengezaji na waagizaji ,mkaguzi wa vifaa wa UNBS,Bw John Sanyu,aslisema wameona matatizo mengi katika baadhi ya maski ambapo watengenezaji wanatumia gundi kushikanisha nyuzi za kufungia kwenye kichwa huku wengine wakitumia vitambaa ambavyo havijapendekezwa.

Bw sanyu alisema lazima kuwe na viwango vinavyokubalika ,na kutoa onyo kwa watengenezaji watakaosambaza maski zenye kasoro kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.