SOKA: Manchester City yapongezwa na timu pinzani
2021-02-19 16:59:39| CRI

Kocha wa Everton Carlo Ancelotti ameipongeza Manchester City na kuweka wazi kuwa timu hiyo ni imara kwenye kila idara, baada ya kikosi chake kupoteza kwa mabao 3-0 usiku wa jana, kwenye mchezo wa ligi kuu England na ushindi huo unaifanya Man City kuongoza ligi kwa tofauti ya alama 10. Vinara wa EPL Manchester City wametengeneza tofauti ya alama 10 kati yao na majirani zao Manchester United wanaoshika nafasi ya pili, baada ya matajiri hao wa jiji la Manchester kushinda mchezo wao wa 12 mfululizo kwa kuinyuka Everton mabao 3-0. Kufuatia kikosi chake kukubali kipigo hicho kocha wa Everton raia wa Italia Carlo Ancelotti, alisistiza kuwa Man City ni timu imara kwa sasa.