Mashimo yasiyotumika uchimbaji yafukiwa
2021-02-19 18:19:24| CRI

Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mgodi  mdogo wa Mwime katika eneo la Kahama mkoani Shinyanga nchini Tanzania wameanza kufukia mashimo yaliyopo katika eneo hilo ambayo yameachwa bila shughuli za uchimbaji kuendelea. Ofisa wa Mawasiliano wa Mgodi huo Christopher Bundala amesema waliamua kuchukua hatua hiyo kwa kuwa huenda yakahatarisha maisha ya watu na hadi kufikia sasa wamefukia mashimo hayo kwa asimilia 90. Aidha Bw Bundala ameongeza kuwa bado wanakumbwa na changamoto nyingi.  Bundala amesema kuwa mashimo hayo yalibaki kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo wahusika kuishiwa mitaji.  Alisema kuna mashimo mengine yamechimbwa na kufikia mita 80, hali ambayo katika zoezi la kuyafukia kunahitaji rasilimali fedha ikiwamo muda ili kuyafukia, hivyo kuepusha majanga yasiokuwa ya lazima kutokea kama vile watu kufukiwa.

Bundala alisema kazi hiyo wanaifanya kwa thadhari kubwa  kwa kufuata agizo kutoka katika ofisi ya madini, ikiwamo kuyatia alama mashimo hayo.