Kampuni za tumbaku zaonywa dhidi ya kuajiri watoto
2021-02-19 18:20:54| CRI

Kampuni za kununua zao la tumbaku nchini Tanzania zimeonywa dhidi ya kuwaajiri watoto katika mashamba ya tumbaku. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kampuni ya Alliance one, David Mayunga amesema badala yake watoto hao wanatakiwa kutumia muda huo kwenda shule.

Mayunga alisema kitendo cha wakulima kuwatumikisha watoto katika mashamba yao hakikubaliki kwa kuwa muda huo wanapaswa kwenda shule ili kutimiza ndoto zao.

Alisema wakulima ambao wako chini ya Kampuni ya Alliance one, wasithubutu kuwatumikisha watoto kwa kuwa ikibainika wanafanya hivyo, tumbaku wanayozalisha haitanunuliwa.

Mkurugenzi huyo aliwahimiza wakulima wa zao hilo kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo yao ya kilimo hekari moja kwa miti 600 ili kulinda mazingira katika maeneo hayo.