Uchumi wa Zimbabwe wakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 7.4 katika mwaka 2021
2021-02-19 16:55:04| cri

Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe Bw. John Mangudya amesema, pamoja na athari mbaya ya janga la COVID-19, uchumi wa Zimbabwe bado unatarajiwa kuongezeka kwa nguvu kubwa hadi kufikia asilimia 7.2 katika mwaka huu.

Katika taarifa yake ya mpango wa fedha kwa mwaka 2021, Gavana huyo amesema, inakadiriwa kuwa uzalishaji wa kilimo utaongezeka katika mwaka 2021 kutokana na msimu mzuri wa mvua, utulivu wa kifedha na ufuatiliaji wa Benki Kuu juu ya utulivu wa bei na mfumo wa kifedha.

Pia alisema kuongeza uzalishaji na tija ni muhimu kwa kudumisha ukuaji wa uchumi wa asilimia 7.4 katika mwaka huu, na zaidi ya asilimia 5 katika siku za baadaye.