Zimbabwe yaanza zoezi la kutoa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na China
2021-02-19 09:42:48| CRI

 

 

Zimbabwe imeanza zoezi la kutoa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na China kote nchini.

Makamu wa rais na waziri wa afya wa nchi hiyo Constantino Chiwenga amekuwa mtu wa kwanza kupata chanjo hiyo nchini humo, na kuwahimiza Wazimbabwe wajitokeze kupata chanjo hiyo ambayo ameitaja kuwa ni salama na yenye ufanisi.

Baada ya kupata chanjo hiyo iliyotengenezwa na Kampuni ya Sinopharm ya China, Chiwenga amesema wizara ya afya ya Zimbabwe imethibitisha ufanisi wa chanjo hiyo kwa njia mbalimbali.

Chanjo ya COVID-19 iliyotolewa kama msaada na serikali ya China ilifika Zimbabwe tarehe 15, na ilianza kutolewa jana alhamis kwa madaktari na wauguzi walioko mstari wa mbele na wafanyakazi wengine walio hatarini zaidi.