Jeshi la Somalia lazima shambulizi katika moja ya kambi zake mjini Mogadishu
2021-02-19 18:20:18| cri

Jeshi la serikali ya Somalia limezima shambulizi katika moja ya kambi zake zilizoko mjini Mogadishu mapema leo.

Waziri wa Habari wa Somalia Osman Dubbe amesema katika taarifa yake kuwa, moja ya kambi zake ilishambuliwa na wapiganaji waliokuwa na silaha, lakini kabla ya shambulizi hilo, walipokea taarifa kuwa kuna shambulizi limepangwa dhidi ya moja ya kambi zake mjini Mogadishu. Lakini Dubbe hakusema kama kuna vifo ama majeruhi yaliyotokana na majibizano ya risasi katika shambulizi hilo.