MIELEKA: Timu ya Mieleka Tanzania yaomba kungwa mkono
2021-02-19 17:00:12| CRI

Serikali na wadau wa Michezo wameombwa kujitokeza kuisaidia timu ya Taifa ya Mieleka inayojiandaa na mashindano mbalimbali ya kimataifa. Timu hiyo inaendelea na mazoezi Msasani Beach jijini Dar es Salaam ikijiandaa na mashindano ya kufuzu kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika April 2 hadi 4, mwaka huu, na ya Ubingwa wa Afrika itakayofanyika Aprili 6 hadi 11, mwaka huu, nchini Morocco. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mileleka ya Ridhaa Tanzania (TAWF), Abraham Nkabuka, ametaja mahitaji yao ni kupata fedha za kujikimu, usajili wa ushiriki, nauli ya kwenda na kurudi na vifaa vya mazoezi.