Afrika kupigwa jeki katika utengenezaji na uunganishaji magari
2021-02-19 18:19:53| CRI

Utengenezaji na uunganishaji magari barani Afrika unatarajiwa kupigwa jeki baada ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya benki ya Afreximbank na chama cha watengenezaji magari Afrika AAAM kufadhili na kupiga jeki sekta hiyo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, mashirika hayo mawili yatashirikiana katika kuongeza thamani kwa kufanya kazi kwa karibu na shirika la kimataifa la OEM ambalo pia litafanikisha juhudi za kutafuta soko. Aidha shirika hilo pia linapanga kufanya utafiti zaidi wa kuchunguza baadhi ya maeneo ambayo yanauwezo wa kutengeneza vipuri kwa ajili ya kufanikisha mpango huo. Benki hiyo inatarajiwa kutoa mikopo ya moja kwa moja kufadhili miradi yote ya utengenezaji magari BARANI Afrika.